Unordered List

Definition List

Jackline Wolper: Lazima Niolewe Nje Ya Nchi

Na Hamida Hassan

STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ameibuka na kudai kuwa, atafanya kila njia ili aolewe na mwanaume wa nje ya nchi na siyo Wabongo ambao hawathamini mastaa.

Akizungumza na Uwazi, Wolper alisema, amefikia uamuzi huo kwa sababu ana uchungu moyoni unaotokana na dhana waliyonayo wanaume wa Kitanzania juu yao, wakiamini kuwa ni wahuni tu hivyo kuwashusha thamani.

“Unajua Mtanzania anamchukulia staa kama chombo cha starehe tu na hawezi kumuoa kamwe na hata akimuoa basi hatamthamini kama wanavyothaminiwa wasanii wa huko nje.

“Kule bwana (hajataja nchi) mtu akimuoa staa, anampa kipaumbele. Anaweza hata kutumia fedha kuhakikisha anakuwa na staa na maisha ya mke wake yanakuwa yenye amani lakini hapa kwetu tunadharaulika sana ndiyo maana nimefikia uamuzi huu,” alisema Wolper na kuongeza:

“Unajua Watanzania wanaamini staa kuandikwa magazetini ni uhuni lakini wanasahau kuwa maisha yake na magazeti ni kitu cha kawaida kwa sababu ya kujulikana. Mimi sina haja ya kueleza sana lakini naapa kabisa, mimi siwezi kuolewa na Mbongo.”
GPL
Jackline Wolper: Lazima Niolewe Nje Ya Nchi Jackline Wolper: Lazima Niolewe Nje Ya Nchi Reviewed by Admin on Tuesday, March 18, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.