Unordered List

Definition List

Utumizi Wa Simu Umekuwa Muhimu Kuliko Tendo La Ngono

Simu ni kifaa ambacho kinasaidia mwanadamu katika shughli zake za kila siku maishani kama vile mawasiliano, kurahisisha kazi katika mambo kadhaa na kadhalika.

Lakini mwendo wa matumizi za simu unakuja kwa kasi kiasi cha kuwa kuna mambo muhimu ya tangu jadi nyakati za akina babu zetu walikuwa wakifanya hivi sasa hayafanywi tena ama mambo hayo yamepunguzwa.

Katika utafiti uliofanywa nchini marekani na Harris Interactive Poll ni kuwa matumizi ya simu yamekuwa muhimu kuliko tendo la ngono.

Asilimia 26 ya wahojiwa wamedai hawawezi kuishi bila simu zao ilihali asilimia 20 pekee ya wahojiwa wamedai kuwa hawawezi kuishi bila tendo la ngono. Na asilimia kubwa ya 28 inasema kuwa hawawezi kuishi bila mtandao wa internet.

Hapa siwezi kusema inaashiria ulimwengu mzima kuwa wamezuzuliwa na simu kiasi cha kusahau mambo mengine. Utafiti huu ulifanywa Marekani na pia ni watu wachache ndio walioweza kuhojiwa. Kwetu Afrika naweza kusema mambo yanaweza kuwa tofauti.

Hebu cheki baadhi ya mambo mengine ya kushangaza kuhusu kizazi hiki cha 'utandawazi'. Utafit uliotengenezwa na Statista - mambo kama haya yanapatikana Marekani pekee...ama wasemaje?


Utumizi Wa Simu Umekuwa Muhimu Kuliko Tendo La Ngono Utumizi Wa Simu Umekuwa Muhimu Kuliko Tendo La Ngono Reviewed by Admin on Tuesday, March 18, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.