Unordered List

Definition List

Masharti 3 Aliyoyakiuka Chris Brown Hadi Kutiwa Jela. Wayajua?

Chris Brown aliweza kufukuzwa kutoka rehab siku ya Ijumaa kwa kukiuka mikataba iliyowekewa na koti.

Msanii huyu mwenye miaka 24 alipewa masharti kuwa asikaribie mwanamke yeyote kwa umbali wa futi mbili wakati wowote kwa sababu kuu ya kuwa ashawahi kumpiga Rihanna wakati mmoja.

Sharti la kwanza alilolikiuka staa huyu ni kumgusa mwanamke mmoja kwa mikono. Hili sharti naliona ni gumu na naona kama wamemuonea hapa.

Sharti la pili alilolikiuka staa huyu ni kuwa kuna wakati alipewa nafasi ya kujiunga na marafiki zake nje ya rihab lakini wakati wa kurudi alikataa kabisa kupimwa kama ametumia madawa yeyote ya kulevya.

Inasemekana ijapokuwa alipita mtihani wa kupimwa kama ametumia madawa ya kulevya, lakini kwa sababu alikataa kupimwa mara ya kwanza, staa huyu wa nyimbo za RnB aliweza kuhukumiwa.

Sharti la tatu aliloweza kulikiuka staa huyu ni kuwa alikejeli zoezi lote la kuwa katika rehab, jambo lililomfanya kuwa hatiani.

Chris Brown sahizi yuko jela kwa kuyakiuka masharti yake na muda huu anangojea mashtaka yaj\ke yafanyike akiwa ndani ya korokoro.
Masharti 3 Aliyoyakiuka Chris Brown Hadi Kutiwa Jela. Wayajua? Masharti 3 Aliyoyakiuka Chris Brown Hadi Kutiwa Jela. Wayajua? Reviewed by Admin on Tuesday, March 18, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.