Unordered List

Definition List

Mtangazaji Mwenye Sauti Ya Kimahaba Diva Loveness Aanika Mapaja Yake Kwa Mtandao

Mtangazaji wa kipindi cha mahaba kiitwacho Ala za Roho kupitia Radio Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ hivi karibuni alilazimika kuyaanika maungo yake ya sehemu za mapaja kushuka chini baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mmoja wa mashabiki wake.

Kupitia blog yake, Diva alidai kuwa siku za nyuma kuna mtu aliomba kuona sehemu hizo za mwili wake hivyo baada ya kum'bania sana ameamua kumtimizia haja yake ili afurahi.

“Kuna mtu alikuwa akidai hajawahi kuona miguu yangu iko ikoje na kwamba nimekuwa nikionesha sehemu ya shingo tena kwa upande, leo nimeamua kumfurahisha,”alisema Diva.

Sambamba na maneno hayo, mtangazaji huyo alijifotoa picha zilizoacha wazi sehemu kubwa ya mapaja yake kisha kuziweka kwenye ukurasa huo.

Diva ni mtangazaji mwenye sauti ya kimahaba, yenye uwezowa kumtoa nyoka pangoni ambaye watu wengi wamekuwa na hamu ya kumuona jinsi alivyo kwani wamezoea kumsikia redioni tu.
Mtangazaji Mwenye Sauti Ya Kimahaba Diva Loveness Aanika Mapaja Yake Kwa Mtandao Mtangazaji Mwenye Sauti Ya Kimahaba Diva Loveness Aanika Mapaja Yake Kwa Mtandao Reviewed by Admin on Wednesday, July 30, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.