Unordered List

Definition List

IRENE UWOYA AFUNGUKA JUU YA TUHUMA ZA KUFANYA FUJO NYUMBANI KWA MUME WA MTU


Nyota wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya amefunguka juu ya tuhuma za kufanya fujo nyumbani kwa mume wa mtu zilizoripotiwa na mitandao mbalimbali ya habari nchini hivi karibuni.


Akizungumza exclusively nasi, Irene amesema kuwa haelewi hizo tuhuma zimetoka wapi na wala hajui aanzie wapi kuzijibu maana siyo yote yaliyoripotiwa ni kweli.
Tuhuma hizo zilidai kuwa, mwanadada huyo mrembo alienda kuleta timbwili nyumbani kwa mume wa mtu huyo baada ya kusikia kuwa jamaa huyoa ameamua kuoa na kumoiga chini Irene aliyekuwa akitoka naye kipindi cha nyuma.

 “Uwoya alitegemea angeolewa yeye, sasa kusikia jamaa kaoa mwanamke mwingine tena kwa siri, ilimfanya aishiwe nguvu,” Habari hizo ziliriripoti.
Habari zinazidi kudai kwamba, alichoamini Uwoya ni kwamba kitendo cha mwanaume huyo kuoa kingemfanya yeye aendelee kuwa ‘nyumba ndogo’ jambo ambalo hakupenda kulisikia hata kidogo.
Akifafanua tukio hilo Zaidi uwoya alisema.
“Ilitokea, lakini nilishaachana naye. Unajua ishu si kwamba angenioa mimi, ila kitendo alichokifanya hakikuwa cha uungwana,” alisema Uwoya.
IRENE UWOYA AFUNGUKA JUU YA TUHUMA ZA KUFANYA FUJO NYUMBANI KWA MUME WA MTU IRENE UWOYA AFUNGUKA JUU YA TUHUMA ZA KUFANYA FUJO NYUMBANI KWA MUME WA MTU Reviewed by Admin on Friday, July 18, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.