Unordered List

Definition List

Ali Kiba Aapa Kuishangaza Bongo Wakati Wa Uzinduzi Wa Nyimbo Zake Mpya


USIPIME! Habari ya mjini kwa sasa ni uzinduzi wa nyimbo mbili za Ally Saleh ‘Ali Kiba’, Mwana na Kimasomaso ambazo atazizindua kwenye Tamasha la Matumaini Agosti 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Kiba ambaye ni mkongwe kunakomuziki wa Bongo Fleva, amefunguka yeye siku zote kuwa ni staa na huwa hakosei hivyo mashabiki watarajie burudani kali siku hiyo.

Kiba ameizungumzia shoo yake katika tamasha hilo kwamba itakuwa spesho hivyo mashabiki wategemee mambo yafuatayo; Shoo kali katika shoo zake zote huwa habahatishi.

Amekuwa ni msanii wa kwanza kutoka Bongo kwa kupiga idadi ya shoo nyingi nje ya nchi kuliko msanii yeyote hata katika matamasha ya ndani ya Bongo amekuwa akiteka hisia nyingi za mashabiki, kwenye tamasha la Matumaini amesema itakuwa ni zaidi ya burudani.'

Kuchomoka kivingine
Baada ya kukaa kimya kwa muda sasa mfalme huyo mwenye sauti ya ajabu, sauti ya kumfanya kila shabiki aikumbuke inapopotea kidogo, amesema anakuja kivingine ambapo atapiga muziki wake kwa mpangilio maalum kuanzia sauti nzuri ya kuwabembeleza.

Habakishi kitu
Kiba amesema siku hiyo hatabakisha kitu, atazipiga nyimbo zote kali kuanzia zile za zamani kama Single Boy, Dushelele, Mac Muga, Run Duniana nyingine kibao bila kusahau Mwana na Kimasomaso ambazo ndiyo habari ya mjini.

Tamasha hilo linatarajiwa kupambwa na matukio kibao ya kusisimua kama ngumi za wabunge, mechi za mpira wa miguu za wabunge na wasanii wa Bongo Fleva, Bongo Movie bila kusahau burudani nzuri kutoka kwa wasanii wanaotamba katika muziki wa Injili.

Burudani zote hizo kwa pamoja, mashabiki watazishuhudia kwa mtonyo wa shilingi elfu tano tu huku sehemu ya mapato yatakayopatikana ikipelekwa katika mfuko wa elimu nchini
Ali Kiba Aapa Kuishangaza Bongo Wakati Wa Uzinduzi Wa Nyimbo Zake Mpya Ali Kiba Aapa Kuishangaza Bongo Wakati Wa Uzinduzi Wa Nyimbo Zake Mpya Reviewed by Admin on Monday, July 28, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.