Inawezekana umeshawahi kusikia malalamiko ya maprodyuza wa muziki Tanzania kuhusu kutonufaika wanavyostahili kwa kazi wanazowatengenezea wasanii, kama zinavyowanufaisha wenyewe kupitia shows wanazofanya kwa kutumia nyimbo hizo.
Lakini inaonekana kuna kafaida zaidi producer anapofanya kazi na wasanii wakubwa, ukiachilia mbali wimbo kupigwa sana na kumpa ‘credit’ mtengenezaji, lakini kuna uwezekano wa kuweka makubaliano ya malipo tofauti kulingana na ukubwa wa wimbo na hata ukubwa wa jina la msanii pia.
Mfano mzuri ni kupitia kazi mpya ya Diamond ‘Mdogo mdogo’ na ya Ommy Dimpoz ‘Ndagushima’, ambazo zote zimetayarishwa na Tudd Thomas wa Surround Sound Studio. Tudd amesema alilipwa jumla shilingi milioni 4 kwa nyimbo zote mbili. “Kikawaida huwa wanasema sio vizuri kwa kuwa ni biashara lakini mimi niko real, ni two million kwa kila wimbo.”Aliiambia Sunrise ya Times FM.
Pia ameongeza kuwa ilimchukua muda mrefu kuziandaa nyimbo hizo, ‘Mdogo mdogo’ ilimchukua miezi mitatu kutokana na idea hiyo kuwa mpya kwa Platnumz na kwake pia, na ‘Ndagushima’ alitumia miezi miwili.

Producer Tudd Thomas Adai Kulipwa Tsh 4 Milioni Kutengeneza Nyimbo Ya 'Mdogo Mdogo'
Reviewed by Admin
on
Saturday, July 19, 2014
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano