Unordered List

Definition List

Baby Madaha Akiri Kuwa Bila Kutumia Uchawi Katika Sanaa Ya Bongo Hautafaulu

Staa wa kike anayefanya vizuri katika tasnia ya muziki na filamu nchini, Baby Joseph ‘Baby Madaha’ amewatolea uvivu wasanii wenzake kwa kuifumua tasnia hiyo kuwa asilimia kubwa ya wasanii ni washirikina na wanarogana….

Msanii huyo amewashtumu baadhi ya wasanii Bongo kuwa hawawezi kufanya jambo yoyote muhimu bila kufanya ushirikina na wengine hawapendi kuona wenzao wakitoka kimaisha…..

Madaha amefikia hatua ya kufumua ishu hiyo kwa madai kuwa hata kufilisika kwake ghafla kumetokea baada ya aliyekuwa mpenzi wake raia wa Kenya Joe Kairuki kupunguza nguvu ya kumsaidia kisanii na kwamba ilitokana na rafiki zake kumpiga juju….

“Wasanii wenzangu wameniloga.Walikuwa wanaona donge sana Joe alipokuwa akinisaidia. Kiukweli wameniporomosha kabisa. Nilienda kwa mtaalamu akanithibitishia hili. Hata hivyo nimepata mfadhili mwingine. Siwezi kumtaja wasije wakanipiga kipapai tena,” alifunguka staa huyo wa wimbo wa Summer Tyme.

Alisema ushirikina umeifanya tasnia ya sanaa kudumaa kwa kiasi kikubwa na kwamba imani hiyo imesababishwa na wasanii wasio na elimu….

“Wasanii wachawi wapo wengi tu.Yaani unamuona msichana mzuri au mvulana mtanashati msanii kumbe anakesha kwa waganga. Wengi wanasafiri sana kwenda mikoani kuloga wenzao. Sanaa imejaa uchuro mtupu. Kama si kuelemewa na ushirikina basi tungekuwa mbali sana."

“Ushirikina umesababisha pia fitina, majungu na visilani miongoni mwa wasanii. Hatupendani kwa sabab ya mioyo ya kichawi,” Alisema Baby Madaha
Baby Madaha Akiri Kuwa Bila Kutumia Uchawi Katika Sanaa Ya Bongo Hautafaulu Baby Madaha Akiri Kuwa Bila Kutumia Uchawi Katika Sanaa Ya Bongo Hautafaulu Reviewed by Unknown on Wednesday, July 16, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.