Unordered List

Definition List

Ray C Alalamika Kuwa Chid Benz Alimvamia Na Kumpiga


Msanii wa muziki na mmiliki wa Ray foundation, Rehema Chalamila aka Ray C amefunguka kwa kusema kuwa alhamisi (july 10) alivamiwa na kupigwa na msanii Chid Benz.

Akizungumza na bongo5 leo, Ray C amesema kuwa Chid Benz anatafutwa na polisi baada ya kufanya tukio hilo. “kweli alinivamia alhamisi usiku, amenipiga mimi na amefanya uharibifu wa mali, mimi nashangaa usiku navamiwa ata sikujua nani amemuonyesha nyumbani kwangu, mimi nilikuwa namtafuta kwa sababu ya show ya kuelimisha vijana na maswala ya madawa ya kulevya, yeye akalichukulia kivingine kabisa, nahisi amechanganyikiwa na madawa ya kulevya, kweli itakuwa amechanganyikiwa na madawa,hayuko sawa kabisa.

Sasa hivi nina RB yake , kwaiyo anatafutwa na polisi, kokote atakapo kamatwa anawekwa ndani, najua atajifisha lakini iposiku atakamatwa na polisi tu. Watanzania wanatakiwa kushirikia na polisi ili akamatwekwa sasabu Chid hayuko sawa kabisa” Alisema Ray C.
Ray C Alalamika Kuwa Chid Benz Alimvamia Na Kumpiga Ray C Alalamika Kuwa Chid Benz Alimvamia Na Kumpiga Reviewed by Unknown on Tuesday, July 15, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.