Unordered List

Definition List

GPL Yazama Na Kisanga Cha Irene Uwoya Alivyopigana Na Mke Mwenza

NYOTA wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya amesababisha tena !

Safari hii amekinukisha nyumbani kwa mwanaume aliyewahi kuwa mpenzi wake ( jina tunalo) kufuatia jamaa huyo kufunga ndoa na mwanamke mwingine na kumfanya Uwoya kuendelea kuwa ‘ nyumba ndogo ’ .
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilichukua nafasi juzikati, nyumbani kwa mwanaume huyo, Sinza- Mori jijini Dar es Salaam.

MCHEZO ULIVYOKUWA
Chanzo kilidai kwamba , siku ya tukio , Uwoya akiwa na baadhi ya mastaa wenzake ( hawakutajwa) kwenye kambi ya maandalizi ya kurekodi filamu mjini Bagamoyo , Pwani, alipokea simu iliyomnyetishia kuwa , mpenzi wake huyo amefunga ndoa na mwanamke mwingine jijini Mwanza , kwa hiyo yeye alie tu !

UWOYA ACHANGANYIKIWA
“Uwoya alipopata salamu hizo kwa njia ya simu alichanganyikiwa ! Alianza kusema maneno ya kumshutumu waziwazi huku akiangua kilio . Mbaya zaidi aliyemjulisha ishu hiyo alisema ndoa hiyo ilishafungwa na si kwamba ipo kwenye maandalizi .

“Akasema anaondoka kambini kumfuata jamaa yake na kwamba atamtambua kwani nia yake ilikuwa kwenda nyumbani kwake kumfanyia fujo na huyo mke mpya, ” kilisema chanzo hicho cha uhakika . Nyumba anayodaiwa kufanya fujo

AANZIA DUKANI
Chanzo kilizidi kudai kwamba, licha ya wasanii wenzake kumsihi asichukue hatua hiyo anaweza kuishia polisi , Uwoya hakukubali, aliondoka kwa hasira na breki yake ya kwanza ilikuwa kwenye duka kubwa la jamaa huyo lililopo Mikocheni , Dar ambapo alifanya fujo. “Kule alipogundua huyo mwanaume wake hayupo ndiyo akaondoka hadi nyumbani kwake, Sinza ambako aliendeleza fujo zake kwa kutukana na kutishia mambo mengi, ” chanzo kilisema .

HASIRA PEMBENI
Kwa mujibu wa chanzo, ni dhahiri kuwa , Uwoya aliondoka eneo hilo baada ya kuanza ‘ kujaza nzi ’ ( watu kuwa wengi ) ambapo aliondoka mdogomdogo na kamahana hasira utadhani si yeye aliyekuwa akichafua hali ya hewa .

MATEGEMEO YAKE
Habari za ndani ziliendelea kudai kuwa , Irene alishikwa na hasira za jamaa huyo kuoa kwa vile alikuwa akiamini zali hilo lingetua kwake baada ya ndoa yake na msakata kabumbu wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘ Katauti’ kwenda halijojo! “Uwoya alitegemea angeolewa yeye, sasa kusikia jamaa kaoa mwanamke mwingine tena kwa siri, ilimfanya aishiwe nguvu ,” kilisema chanzo.

ALICHOAMINI
Habari zinazidi kudai kwamba, alichoamini Uwoya ni kwamba kitendo cha mwanaume huyo kuoa kingemfanya yeye aendelee kuwa ‘ nyumba ndogo ’ jambo ambalo hakupenda kulisikia hata kidogo .

UWOYA HUYU HAPA
Baada ya gazeti hili kunyetishiwa filamu nzima, lilimsaka staa huyo na kubahatika kukutana naye maeneo ya Sinza Palestina jijini Dar ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba, alishaachana na mwanaume huyo. “Ilitokea, lakini nilishaachana naye . Unajua ishu si kwamba angenioa mimi , ila kitendo alichokifanya hakikuwa cha uungwana , ” alisema Uwoya .

AMWANGA CHOZI
Katika hali isiyotarajiwa , msanii huyo alianza kumwaga chozi bila kusema sababu hata pale alipoulizwa kama chozi hilo lilitokana na kukumbuka tukio la jamaa yake kufunga ndoa kwa siri au la! Uwoya: “We niache tu , nina mambo mengi sana yanayoniliza mimi .” Kwa upande wake mwanaume huyo alipopatikana kwa njia ya simu na kueleza ishu nzima alijibu kwa kifupi: “Haiwahusu.” Kisha akakata simu.
GPL
GPL Yazama Na Kisanga Cha Irene Uwoya Alivyopigana Na Mke Mwenza GPL Yazama Na Kisanga Cha Irene Uwoya Alivyopigana Na Mke Mwenza Reviewed by Unknown on Thursday, July 17, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.