Unordered List

Definition List

Recho: Sina Uhusiano Wa Kimapenzi Na TID


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Winfrida Josephat maarufu kama Rachel, amekanusha uvumi kuwa anatoka kimapenzi na mkongwe wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’.

Rachel ambaye ni zao la Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT), aliyetambana kibao chake cha Kizunguzungu, alisema maneno hayo siyo mageni kwake, lakini ukweli ni kwamba hawana uhusiano wa kimapenzi, isipokuwa amemuweka katika mipango ya kuja kufanya kazi na mkali huyo wa singo iliyotamba sana ya Zeze.

Aidha alisema katika maisha yake ya kila siku, hategemei kuhongwa vitu au hela na wanaume, ila baada ya kupata mafanikio kupitia sanaa, anaitumia kama mtaji wa kufanya shughuli nyingine za kumuingizia kipato na hivyo kuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji yake.
Recho: Sina Uhusiano Wa Kimapenzi Na TID Recho: Sina Uhusiano Wa Kimapenzi Na TID Reviewed by Unknown on Wednesday, July 16, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.