Unordered List

Definition List

Diamond Platnumz Amvisha Pete Wema Sepetu, Ni Ya Uchumba!?


SAPRAIZ! Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu (25) ameibua viulizo baada ya kuonekana akirandaranda na pete ya ndoa kidoleni ikidaiwa kuwa amevalishwa na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa siri kubwa, Ijumaa Wikienda lina stori exclusive.

Baada ya kuwepo kwa habari nyingi kuhusiana na ishu hiyo, Ijumaa Wikienda liliingia mzigoni kusaka ukweli wa ishu hiyo na kujua mbivu na mbichi. Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa mkali huyo wa sinema za Kibongo, hata mashosti zake hawajui kinachoendelea zaidi ya kuulizana wao kwa wao kuhusu nini kinaendelea huku kukiwa na hisia kuwa huenda wawili hao wamefunga ndoa ya siri

HAJAFUNGA NDOA LAKINI…
Wema alisema si kweli kwamba amefunga ndoa ya siri ila Diamond alimvisha pete hiyo kama urembo akijua kabisa kwamba yeye ni wife material (anafaa kuwa mke).“Sijafunga ndoa jamani. Hii pete alininunulia baby wangu Nasibu (Diamond) wakati tukiwa South Africa (Afrika Kusini).

WEMA AIONA PETE, YAMVUTIA
“Alininunulia na kunivisha tulipokwenda kwenye Tuzo za MTV Africa (MAMA). Nakumbuka tuliingia kwenye duka moja nikaiona hii pete ikanivutia sana, nikamwambia Nasibu ndipo akaninunulia na kunivisha palepale.“ Cha kushangaza ni kwamba imewatatiza wengi na kuhisi ndoa tayari. “Hii pete ndogo niliinunua mwenyewe hapa hapa Bongo na kuivaa kama urembo tu, hakuna tofauti na hilo kuhusiana na hizi pete nilizovaa kidole husika,” alisema Wema ambaye kidoleni kwake kunaonekana pete mbili, kubwana ndogo.

WEMA NI WIFE MATERIAL?
Alipoulizwa kwa nini Diamond aliamua kumvisha pete hiyo kabla ya ndoa, Wema alifunguka: “(kicheko) hilo sina uhakika nalo but amegundua mimi ni wife material hataki kunipoteza. Kanipa heshima anayostahili kupewa mwanamke...”
Diamond Platnumz Amvisha Pete Wema Sepetu, Ni Ya Uchumba!? Diamond Platnumz Amvisha Pete Wema Sepetu, Ni Ya Uchumba!? Reviewed by Unknown on Monday, July 21, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.