Unordered List

Definition List

Mama Kanumba Ajeuka Omba Omba Mtaani, Mumewe Amkashifu

BABA wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba ameibuka na kumtaka mama Kanumba, Flora Mtegoa kuacha tabia ya kuombaomba michango mbalimbali.

Akipiga stori na paparazi, Baba Kanumba alisema anashangazwa na tabia ya mama Kanumba kuombaomba ambapo hivi karibuni alimuona mjini Shinyanga ambako alikuwa akiomba rambirambi kwenye kumbi za starehe.

“Namshangaa mama Kanumba ninjaa gani hiyo, naomba aache kudhalilisha ukoo wa Kanumba kwani anatumia jina hilo kuombaomba, anahangaika bila sababu za msingi wakati sisi tuko vizuri,” alisema Baba Kanumba.Mama Kanumba.

Akijibu tuhuma hizo, mama Kanumba alisema kama ana malalamiko yoyote aende mahakamani maana yeye si mume wake. “Aache kunifuatafuata kwani mimi si mkewe na Shinyanga nilialikwa kwenye Miss Shinyanga siyo kwamba nilijiendea tu,” alisema.
Mama Kanumba Ajeuka Omba Omba Mtaani, Mumewe Amkashifu Mama Kanumba Ajeuka Omba Omba Mtaani, Mumewe Amkashifu Reviewed by Unknown on Thursday, July 10, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.