Unordered List

Definition List

RAY ashindwa kumzika “Baba’ke” na JOHARI. Chuchu Hans 'Atajwa'.


MKURUGENZI wa RJ Company, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameshindwa kumzika baba mdogo wa mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo, Blandina Chagula, Clement Kiyenze Chagula.

Mzee huyo alifariki katika Hospitali ya Muhimbili kutokana na matatizo ya presha na figo yaliyokuwa yakimsumbua na kuzikwa katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar ambapo wasanii mbalimbali wa filamu nchini walishiriki akiwemo Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.

Alipoulizwa Ray kwa nini hakuhudhuria mazishi hayo, alisema: “Ukweli ni kwamba mimi sipo Dar. Ndiyo maana sijaonekana huko kwenye mazishi, nipo Mwanza katika shughuli zangu za kikazi, tuko pamoja lakini,”

Ingawa wachunguzi wa mambo wanasema kuwa alikuwepo mjini ila ni kutokana na sababu binafsi zao kati yake na Johari ndo maana hakutaka kwenda huku chuchu hans akidaiwa kuhusika.
RAY ashindwa kumzika “Baba’ke” na JOHARI. Chuchu Hans 'Atajwa'. RAY ashindwa kumzika “Baba’ke” na JOHARI. Chuchu Hans 'Atajwa'. Reviewed by Admin on Friday, July 25, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.