Unordered List

Definition List

Video Game Ya Kim Kardashian Kuvunja Rekodi Ya Kupata $200 Milioni Mwaka Huu

Kama bado hujafahamika ni kuwa Kim Kardashian hivi karibuni alifanya uzinduzi wa video gemu yake. Video hii ambayo sana ni ya fasheni imemfanya Kim kwa mara nyingine kuingia katika nyanja mpya ya kupata kipato kando na ile ya video yake ya ngono.

Video Game hii ya Kim Kardashian imemtajirisha na inaweza kumfanyakuwa miongoni mwa wanawake watatu matajiri zaidi duniani kwenye kiwanda cha burudani kwa mwaka 2014.

Mchambuzi wa Doug Creutz aliimbia Bloomberg kuwa video game hiyo itamuingizia Kim Kardashian kiasi cha $ 200 million, huku ikiwa imeshika nafasi ya kwanza kwenye iTunes na inadaiwa kuwa video game ya kwanza kufikia rate ya nyota 5 mwaka huu.Mchambuzi huyo ameeleza kuwa umaarufu wa jina la Kim Kardashian limewavutia wengi kudownload application hiyo, lakini kwa sasa game hio inaendelea kuwa na umaarufu wake.

Tayari video game hiyo imekuza hisa ya kampuni ya Glu Mobile kwa 42%, na Chief Operating Officer wa kampuni hiyo ameeleza kuwa ni video game kubwa zaidi ya mwaka kwao, “Our biggest game of the year.”

Ingawa inapatikana kwa free, kuna gharama inayotumika ili kuwawezesha wachezaji kununua vitu vya digitali (digital accessories) kwa pesa.
Video Game Ya Kim Kardashian Kuvunja Rekodi Ya Kupata $200 Milioni Mwaka Huu Video Game Ya Kim Kardashian Kuvunja Rekodi Ya Kupata $200 Milioni Mwaka Huu Reviewed by Admin on Tuesday, July 15, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.