Unordered List

Definition List

Davina Wa Bongo Movies Apewa Kichapo Na Mumewe Baada Ya Kufumwa Akiongea Kimahaba Kwa Simu

Na Musa Mateja
KIBANO! Staa wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ anadaiwa kupewa kipigo kikali na mumewe, muda mfupi baada ya kukutwa akiongea kimahaba na simu iliyodaiwa kupigwa na mwanaume mwingine.

Tukio hilo lilitokea nyumbani kwa msanii huyo, Mbezi-Beach, Dar, Julai 22, mwaka huu ambapo Davina alikutwa akizungumza na mwanaume ambaye haikujulikana mara moja ni nani ndipo mumewe alipomshushia kipigo ‘hevi’.

Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu familia hiyo, mume wa Davina aliibua timbwili hilo baada ya kumsikiliza kwa makini mkewe huyo na kugundua anazungumza na mwanaume mwingine wakiahidiana kitu f’lani. “Mumewe alitega sikio kwa makini na kugundua alikuwa akizungumza na mwanaume, akamsogelea karibu na kunasa mazungumzo yao, akamuoma simu mara moja, Davina akaanza kujitetea ndipo mtiti ulipoibuka, mume akaanza kumpiga mke ingawa hakumuumiza kiivyo,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya data hizo kutua kwenye Dawati la Risasi Jumamosi, mwanahabari wetu alimvutia waya Davina ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kufafanua kuwa hakuwa akiongea na mwanaume huyo kwa lengo baya zaidi ya maongezi ya kikazi.

“Dah! Umejuaje hii ishu ni ya kifamilia hivyo! Mmh...kweli ninyi ni noma, anyway ishu ni kwamba, mume wangu alinifuma nikiongea na simu ya jamaa mmoja ambaye alikuwa ananipigia ili anipatia fedha zangu ambazo zilibaki baada yakufanya tangazo moja linalohusiana na mambo ya Ukimwi.“
"Wakati naongea, yeye (mumewe) hakujua nini kinaendelea zaidi alikuwa akisikia sauti ya mwanaume tu na majibu yangu kweli akajikuta amepaniki na kunivaa akiwa ana hasira, si unajua mtu yeyote anayekupenda wivu huwa ni kitu cha kawaida tu lakini nilimwelewesha baadaye akanielewa na maisha yanaendele kama kawaida,” alisema Davina.
GPL
Davina Wa Bongo Movies Apewa Kichapo Na Mumewe Baada Ya Kufumwa Akiongea Kimahaba Kwa Simu Davina Wa Bongo Movies Apewa Kichapo Na Mumewe Baada Ya Kufumwa Akiongea Kimahaba Kwa Simu Reviewed by Unknown on Saturday, July 26, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.