Unordered List

Definition List

Bob Juniour Kuandaa 'Usiku Wa Masharobaro' Kusherehekea Mafanikio Ya Miaka 8


Msanii wa muziki na producer wa Sharobaro Records, Bob Junior amedai anatarajia kufanya show ya usiku wa masharobaro ambapo amedai atatoa tuzo kwa wadau waliomsaidia kufika hapo alipo.

Bob Junior akizungumza na Bongo5 amedai kuwa show hiyo itakayofanyika August 3 mwaka huu itahudhuriwa na wasanii wote waliowahi kufanya ngoma Sharobaro Records.

“Natarajia kufanya show ya usiku wa Masharobaro ndani ya Maisha Club tarehe 3 mwezi wa nane mwaka huu yaani ni show ya kwanza Jumapili Maisha Club tunafungua sisi,” amesema.

“Wasanii wote ambao wamefanya hits kutoka Sharobaro records nitawaalika. Wasanii ambao watanisupport bado sijawapanga. Bob Junior nitafanya show ya kitofauti kabisa na nitatoa certificate au tuzo kwa media zote na namaanisha kuanzia blogs, TV station na redio na magazine. Kwa hiyo kutakuwa na vitu vikubwa sana.”
Bob Juniour Kuandaa 'Usiku Wa Masharobaro' Kusherehekea Mafanikio Ya Miaka 8 Bob Juniour Kuandaa 'Usiku Wa Masharobaro' Kusherehekea Mafanikio Ya Miaka 8 Reviewed by Admin on Saturday, July 26, 2014 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.