Unordered List

Definition List

Khadija Kopa Nusra Apigwe Na Wahuni Baada Ya Kunaswa Na Msenge


MASKINI! Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki na Kati, Khadija Omary Kopa amevamiwa na vijana wahuni wakitaka kumfanyia fujo kwa madai ya kukatiza mitaani akiwa anatembea na ‘mwanaume tata’.

Tukio hilo lilijiri maeneo ya Kariakoo, Dar wiki iliyopita ambapo vijana hao walianza kwa kuzomea wakitaka kumshika mwanaume huyo waliyedai alikuwa amevaa nguo za jinsia ya kike.

Alichokifanya Khadija ni kuingia kwenye gari na kumwambia dereva aondoke haraka kukwepa kufanyiwa vurugu huku mwanaume huyo naye akiungana na malkia huyo kuondoka eneo hilo.

Wakizungumza na gazeti la GPL, vijana hao walidai kuwa Khadija alijiabisha kwa kutembea na mwanaume huyo.

Khadija alimwambia paparazi wa GPL kuwa alishangazwa na tukio hilo lililomkuta na kusema kuwa mwanaume aliyekuwa akitembea naye ni mwimbaji mwenzake ambaye pia ni shemeji yake.

Alifunguka: “Hivi kuwa mwimba taarabu wa kiume ndiyo ushoga jamani? Au kuvaa kaptura ya kitenge ni tatizo? Mbona alikuwa amevaa mavazi mazuri tu ya kiume?”

Khadija alisema kuwa amewazoea mashabiki wake wa Kariakoo kwani huwa wakiwaona mastaa huwa na tabia hiyo na ndiyo maana walianza uzushi huku wakisema kuwa waimba taarabu wote ni wanawake, kitu ambacho si kweli.

“Sikuona sababu ya kuchukua hatua, nilikuwa najaribu kuwaelewesha lakini hawakunielewa, wakazidi kuzomea na kutuzingira ndiyo maana tuliamua kuondoka,” alisema Khadija.

-GPL
Khadija Kopa Nusra Apigwe Na Wahuni Baada Ya Kunaswa Na Msenge Khadija Kopa Nusra  Apigwe Na Wahuni Baada Ya Kunaswa Na Msenge Reviewed by Admin on Monday, December 02, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.