Unordered List

Definition List

Siri Ya Aunty Lulu Yajulikana, Ametundikwa Mimba

 

Baada ya kurukaruka sana, sasa inadaiwa ni mjamzito wa takribani miezi mitano. Akilinyetishia Ijumaa juu ya ishu hiyo, rafiki wa karibu wa Anti Lulu aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema, msanii huyo sasa amekuwa mtumiaji mzuri wa maembe mabichi huku magauni mapana yakiwa ndiyo mavazi yake.

“Mwanzo alikuwa anaficha lakini sasa siyo siri na mwenyewe ameona ni bora kuwataarifu ndugu na marafiki zake,” alisema mtoa habari huyo. Katika kujua undani wa hilo, waandishi wetu walimsaka Anti Lulu na kufanikiwa kumuona akiwa na kitumbo chake lakini akaomba asipigwe picha ila akasema: “Mmechelewa kujua, mbona inakwenda mwezi wa tano sasa, mwenye mzigo mtamjua nikishajifungua jamani,”alisema msanii huyo.
GPL
Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
Siri Ya Aunty Lulu Yajulikana, Ametundikwa Mimba Siri Ya Aunty Lulu Yajulikana, Ametundikwa Mimba Reviewed by Admin on Saturday, December 07, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.