Unordered List

Definition List

Sehemu Ya Kufanya Ndoa Ya Kim Kardashian Na Kanye West Ishajulikana!!!

kim kardashia na kanye west
Tetesi zote kuwa ndoa ya Kimye itahairishwa inaelekea kuwa tetesi yenyewe.

Hii ni baada ya dalili zote kuonyesha kuwa wawili hao wako tayari kufanya ndoa yao. Kimye tayari washasema kuwa ndoa yao wataionyesha kwa runinga, pia Kanye aliweza kumpigia magoti Kim kutaka wafanye ndoa.

Na hivi sasa...

Kim na Kanye tayari inaonekana washasema mahali watakapofanya harusi yao...harusi yenyewe itakuwa ya kifalme.

Kulingana na gazeti la Us Weekly, wawili hao wanataka kufanya harusi yao nchini Ufaransa katika jumba la kifalme la Varsailles.

"Kanye ni mara yake ya kwanza kufanya harusi, kwa hivyo anataka harusi yake iwe ya juu na ya kifahari" jarida moja lilisema.

Kanye mwezi wa Oktoba aliweza kumwomba Kim amuoe na aliwaalika zaidi ya watu 50 wamuimbie huku akiweka bango kubwa na maandishi" PLEEEASE MARRY MEEEEE".

Tegea matukio yote yanayowahusu familia ya Kim Kardashian hapa
Sehemu Ya Kufanya Ndoa Ya Kim Kardashian Na Kanye West Ishajulikana!!! Sehemu Ya Kufanya Ndoa Ya Kim Kardashian Na Kanye West Ishajulikana!!! Reviewed by Admin on Sunday, December 08, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.