Unordered List

Definition List

R.I.P Lil Wayne Ulikuwa Uvumi Wa Mtandao

Siku ya jana Ijumaa nne haikuwa nzuri kwa msanii Lil Wayne baada ya uvumi wake kuwa amefariki. Uvumi huo chanzo chake kilianza katika mtandao wa Facebook ambapo kulikuwa na kitumizi ambacho kilikuwa kikisambaza uvumi kuwa Lil Wayne amefariki.(tofauti na hio video ya hapo chini)


Katika video iliyokuwa ikienezwa kwa Facebook ikiwa na jina 'R.I.P. Lil Wayne. Rapper Found Dead' imeshtua mafans wake wengi wa mwanamziki huyu.

Ukweli ni kuwa rappa huyu ameshawahi kujitokeza wazi na kusema kuwa yeye ana ugonjwa wa kifafa na mara kwa mara ameshawahi kuugua ugonjwa huu na anaweza kushikwa nao mahala popote.

Mitandao kadhaa ya udaku ilikuwa ikieneza habari kuwa Lil Wayne anafanyiwa matambiko yake ya mwisho baada ya kushikwa na kifafa.

Lakini stori hio imeshabainishwa wazi kuwa ni uvumi tu, kwani Lil Wayne hivi juzi tu ametoa video mpya na Chris Brown.
R.I.P Lil Wayne Ulikuwa Uvumi Wa Mtandao R.I.P Lil Wayne Ulikuwa Uvumi Wa Mtandao Reviewed by Admin on Wednesday, December 18, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.