Unordered List

Definition List

Ali Kiba Kurudi Kwa Game, Amechelewa?!?

Hitmaker wa Cinderela na Dushelele, Ali Kiba ambaye jana alisherehekea birthday yake ya kutimiza umri wa miaka 27, amefunguka kwa kusema alikuwa kimya kutokana maisha ya muziki anayosema yamejaa drama, mateso na mambo mengi.

Akizungumza na Bongo5 jana, Ali Kiba amesema muziki wa Tanzania umejaa drama zilizomfanya atulie kidogo kutafakari na ili kusudi ajue jinsi ya kukabiliana na changamoto zake.

“Nashukuru Mungu nimetiza miaka 27, ni wakati wangu wa kuamka katika usingizi uliyojaa maumivu,drama na mambo mengi ambayo yameweza kunikalisha kimya. Sitaki kusema moja kwa moja kwamba nilikuwa kimya kwa sababu maalum ambayo hata ingemkuta mwingine lazima angetulia,” Ali Kiba aliiambia Bongo5.

“Namalizia audio na video ambazo ni kali sana. Unajua nimekuwa nikipokea maoni mengi kwenye Twitter, Instagram na baadhi ya rafiki zangu wakinitaka niamke nifanye mambo. Kwahiyo nadhani muda wangu umefika wa kuamka na kufanya yale mambo ambayo nilikuwa nayafanya. Huu ni muda wa kutoka kutoka nilipokuwa.”

Happy Birthday Ali K and welcome back.
Credit-BONGO5.COM
Ali Kiba Kurudi Kwa Game, Amechelewa?!? Ali Kiba Kurudi Kwa Game, Amechelewa?!? Reviewed by Admin on Sunday, December 01, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.