Unordered List

Definition List

Masogange Yuko Dar, Ajificha Asionekane Na Mapaparazi

VIDEO Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ ambaye alipata soo la kukamatwa na malighafi haramu aina ya Ephedrine Julai 5, mwaka huu nchini Afrika Kusini na pia staa ambaye anaiteka hisia za mashabiki wake kwa kuweka picha za nusu utupu amejaa tele jijini Dar es Salaam, Ijumaa limethibitisha.

Masogange ambaye siku ya tukio alikuwa na nduguye, Melisa Edward baada ya kunaswa na madawa hayo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park jijini Johannesburg nchini humo alihukumiwa kwenda jela miezi 32 au kulipa faini ya shilinghi milioni 4.8 ambapo aliweza kulipa na kuwa huru.
Masogange akiwa na Jack Patrick

Tangu aachiwe huru, Septemba mwaka huu, msanii huyo akawa hajulikani alipo huku baadhi ya ‘posti’ zake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram zikionesha yupo Tanzania au Afrika Kusini.
Masogange akipozi dukani Bongo.

Jumatatu iliyopita, mida ya saa kumi jioni, paparazi wetu alipigiwa simu na msomaji wa gazeti hili (jina tunalo) akisema amemwona Masogange akiingia kwenye duka la nguo lililopo Sinza Kamanyola, Dar akiwa peke yake.

Paparazi wetu alijipanga kwa kamera na kutia timu kwenye duka hilo ambapo hata hivyo muuzaji alisema aliondoka baada ya kufanya manunuzi ya kawaida.

Jumatano, Masogange alitumbukiza picha kwenye mtandao wake akiwa ndani ya duka hilo na modo maarufu nchini, Jacqueline Patrick.

Jack alipigiwa simu ambapo alikiri kuwa na Masogange siku ya Jumanne kwenye duka hilo. Akasema: “Mimi nilimkuta pale, tukapiga picha tukaachana, basi.”

Kwa kutumia namba yake ya simu ya mkononi, Masogange alipatikana na kukiri yupo Dar lakini akasema hakutaka kuweka wazi kwa sababu anawaogopa sana mapaparazi.

-Global Publishers
Masogange Yuko Dar, Ajificha Asionekane Na Mapaparazi Masogange Yuko Dar, Ajificha Asionekane Na Mapaparazi Reviewed by Admin on Saturday, November 30, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.