Unordered List

Definition List

Filamu Ya After Death Ya Kumuenzi Kanumba Ilikuwa Hasara Tupu, Wolper Afunguka

NYOTA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa filamu yake aliyoitoa kumuenzi marehemu Steven Kanumba iitwayo After Death ilimpatia hasara kubwa.

“Nilitengeneza ile filamu kwa hela nyingi kidogo, kama milioni 35 au 40, nikafanya na uzinduzi pale Leaders Club uliogharimu kama milioni 13 hivi, lakini nilipokwenda kwa Wahindi wakanipa shilingi milioni 25, yaani inakatisha sana tamaa,” alisema muigizaji huyo wakati alipofanya mahojiano maalum na waandishi wetu.

Alisema hasara aliyoipata na ambayo hata wasanii wenzake huipata inatokana na uwepo wa wasambazaji wachache wa kazi za wasanii, kitu kinachowafanya watu hao kujipangia bei bila kujali gharama ambazo wameingia katika utengenezaji wake.

Chanzo: GPL
Filamu Ya After Death Ya Kumuenzi Kanumba Ilikuwa Hasara Tupu, Wolper Afunguka Filamu Ya After Death Ya Kumuenzi Kanumba Ilikuwa Hasara Tupu, Wolper Afunguka Reviewed by Admin on Saturday, November 30, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.