Imeandikwa na Warumi Warumi
Kile kipindi ambacho bifu la Clouds Media Group na mwanamuziki Lady Jaydee lilipopamba moto, ambapo bifu lilikuwa kali kweli kweli, ndipo msanii Lady Jaydee baada ya kuhisi kuzidiwa na radio hiyo, aliamua kuunda TEAM aliyoipa jina la ANACONDA TEAM au TEAM ANACONDA.
Team ambayo haikumuangusha hata alipofanya ile show ya kutimiza miaka kumi na tatu kwenye muziki,ambapo mashabiki au team ya Lady Jaydee ilionyesha ushirikiano kwa asilimia zote. Lady Jaydee ndiye msanii aliyeanzisha kundi la ushabiki(TEAM), ambapo baadhi ya wasanii huitumia vibaya, nadhani lengo lake halikuwa baya kwani alitumia mbinu hiyo ili kuinua soko lake la muziki.
Siku hizi imekuwa kama FASHION, baadhi ya mastaa wakigombana basi kinachofanywa ni kuundwa TEAM ambapo mashabiki wa wasanii hao huingilia kati bifu la wasanii hao na kuanza kuwarushia matusi mazito mitandaoni wapinzani wao, unakuta bifu linaweza kuwa la kawaida ila mashabiki wanalikuza na kujifanya wenyewe ni team flani na kuanza mshambulizi mitandaoni,mfano juzi ile ishu ya ray na wema kuna mdada mtandaoni ambaye anatumia username TEAMWEMASEPETU alimtukana matusi ya nguoni Ray, yaani kwa namna nyingine kanunua bifu, kitu ambacho sio kizuri, hivi karibuni tena baada ya kutokea bifu kati ya Johari na Mainda baadhi ya mashabiki wa Johari wanaojiita TEAM JOHARI walimporomoshea matusi mazito Mainda kwenye mtandao wa instragram, vile vile TEAM MAINDA haikuwa nyuma ilirudisha matusi hayo, yaani imekuwa bifu la mashabiki wa fulani na fulani sio wasanii hao tena, kitu ambacho sio kizuri kwa wasanii.
Kuna baadhi ya wasanii huunda TEAM kwa nia njema tu, mfano feza kessy alipokuwa mjengoni aliunda TEAM FEZA, akiwahimiza mashabiki wake kumpigia kura,something which is good. salute kwa LADY JAYDEE na TEAM ANACONDA-THE LEADING TEAM IN TOWN

Chanzo Cha Bifu La Neno Team...
Reviewed by Unknown
on
Wednesday, November 20, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano