Unordered List

Definition List

MILEY CYRUS Alivuta Bangi Jukwaani, Sasa Uchunguzi Waanza

Miley Cyrus na Bangi
Serikali ya Uholanzi imeanza uchunguzi rasmi kuangalia kama ni ukweli msanii wa Marekani Miley Cyrus aliwasha msokoto wa bangi alipokuwa kwa jukwaa wakati wa MTV Music Awards jijini Amsterdam.

"Tumepata malalamishi kuwa msanii huyu aliwasha bangi alipokuwa juu ya jukwaa na tumeanzisha uchunguzi wetu" Tjitte Mastenbroek mkuu wa Usafi wa Vyakula kwa Umma aliongea.

Msanii Miley Cyrus mwenye tetesi nyingi baada ya kutoa video ya uchi akiwa akiimba nyimbo ya 'Wrecking Ball' aliwasha msokoto wa bangi katika tuzo la MTV wakati wa kupokea tuzo la video bora ya 'Wrecking Ball'.

Inakisiwa kuwa Miley amechukizwa sana na vile watu wanavyomuona kama mtoto mdogo kwa kuwa alikuwa staa katika kipindi cha Hanna Montanna.

Hatua sasa anazichukua ni kujitenganisha yeye na Hanna Montanna, inadadisiwa kuwa atatoa filamu ya ngono hivi karibuni.


MILEY CYRUS Alivuta Bangi Jukwaani, Sasa Uchunguzi Waanza MILEY CYRUS Alivuta Bangi Jukwaani, Sasa Uchunguzi Waanza Reviewed by Admin on Monday, November 18, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.