Unordered List

Definition List

Tendo La Ngono Litakuua, Utafiti Wabainisha

Tengo La Ngono Litakuua, Utafiti Wabainisha
Kwa muda mrefu watu walikuwa wakijiuliza maswali kama iwapo kufanya ngono kunaweza kuathiri mtu kushikwa na mshtuko wa moyo(heart attack).

Kulingana na jarida kutoka mtandao wa Reuters, utafiti wa Marekani umebainisha kuwa ni kweli kufanya tendo la ngono linaweza kukuua.

Utafiti uliofanywa marekani umebainisha na kugundua kuwa watu wanaojamiiana wana athari ya kushikwa na mshtuko wa moyo mara 2.7 kuliko na wale hawafanyi tendo hilo.

Utafiti pia uliofanywa mwaka wa 1996 na kikundi kimoja cha Havard, kilibainisha kuwa athari ya kushikwa na mshtuko wa moyo huongezeka mara dufu kwa wale ambao wana historia ya maradhi ya ugonjwa wa moyo(coronary heart disease).

Sasa ule uvumi wa kuwa tendo la ngono huua umebainishwa lakini wanasayansi tofauti wanadai kuwa ni asilimia ndogo sana kwa mtu kupatikana na athari hio na jambo hilo halifai kushtua mtu na maisha yake ya kujamiiana.

Hii ni changamoto kwa kila mmoja kuuchunga moyo wake vyema na kuishi maisha ambayo hayata muathiri maisha yake ya usoni.


Tendo La Ngono Litakuua, Utafiti Wabainisha Tendo La Ngono Litakuua, Utafiti Wabainisha Reviewed by Admin on Saturday, November 09, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.