Unordered List

Definition List

Wema Sepetu Kumlipia Kajala 13 Milioni

Kajala Masanja.
AMA kweli hujafa hujaumbika! Bado bundi anamnyemelea staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja baada ya kurejeshwa kortini kwa mara nyingine huku kesi ikimjia upya, Risasi Mchanganyiko limesheheni.
MUME AKATA RUFAA
Pamoja na kutoa faini ya Sh. milioni 13 alizolipiwa na staa mwenzake wa filamu, Wema Isaac Sepetu, Kajala anatarajiwa kuhukumiwa tena Novemba 25, mwaka huu baada ya mumewe, Faraji Agustino Chambo kukata rufaa katika mahakama kuu.
Kwa mujibu wa jaji aliyezungumza na gazeti hili, kuna kila dalili wawili hao wakaachiwa huru au wakafungwa tena kwa adhabu kubwa zaidi ya ile ya awali, hivyo huu ni msala mpya kwa Kajala ambaye tayari alikuwa uraiani.
Kajala na mumewe, Faraja Chambo wakisubiri siku ya  hukumu yao.
Kesi iliyokuwa ikiwakabili wanandoa hao ilihusiana na utakatishaji wa fedha haramu uliofanywa na mume wa Kajala wakati akifanya kazi kwenye Benki ya NBC, Dar.
Mume wa staa huyo ndiye anadaiwa kukata rufaa wakati akitumikia kifungo cha miaka saba jela baada ya kukutwa na hatia.
Habari za ndani zilieleza kwamba, Kajala alisharidhika na hukumu iliyotolewa Machi 25, mwaka huu ambapo yeye  alitakiwa kufungwa mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni 13.
Wema na Kajala.
Katika hukumu hiyo, mume wa Kajala alifungwa miaka saba na ndipo alipoamua  kukata rufaa na akamuingiza Kajala kwa maelezo kuwa wote hawakuridhishwa na hukumu iliyotolewa mwanzoni.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Kajala, staa huyo amekuwa katika wakati mgumu na mara nyingine na kujikuta akiangua kilio hasa anapokumbuka maisha ya gerezani.
Baba Kajala (kushoto) akishauriana jambo na wasanii wa filamu na maswahiba wa mwanaye siku ya hukumu ya mwanae.
KAJALA KORTINI
Ili kuthibitisha habari hizo, juzi (Jumatatu) Kajala akiwa na shosti wake, Wema anayehaha kumnasua, alipigwa chabo na mashushushu wetu wakitinga tena katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Habari zilieleza kuwa jaji ambaye alikuwa akipitia ya hukumu ya awali ya wanandoa hao, alidai kwamba  Jaji Temba aliyetakiwa kutoa hukumu ya kesi hiyo upya alikuwa anaumwa.
HUKUMU NOVEMBA 25
Kufuatia kuumwa kwa hakimu huyo, kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 25, mwaka huu, ambayo itakuwa siku ya hukumu huku ikielezwa kuwa kila kitu kipo tayari.
Akiwa katika viunga vya mahakama hiyo, Kajala alionekana mwenye wasiwasi na woga kwa sababu hakuwa anajua kama anaweza kuburuzwa kortini kwa mara nyingine kuhusiana na suala hilo kwa kuwa aliamini alishamaliza kwa kulipa faini ya Sh. milioni 13 kisha kurejea uraiani huku mumewe akienda jela.
Kajala alisema anaomba Mungu ili kikombe hicho kimuepuke kwani alishasahau kama anaweza kurudi kortini.
“Sikudhani kwa kweli kama ninaweza kurudi mahakamani, Mungu anisaidie kwa kweli…” alisema Kajala.
Naye Wema alipigwa na mshangao baada  ya kuona kesi hiyo imeibuka tena.
“Siku ile niliuliza kilikuwa kinahitajika nini ili Kajala awe huru, nikaambiwa milioni 13, nikatoa, sasa iweje tena arudishwe mahakamani?” alihoji na kuonesha wasiwasi mkubwa baada ya kuambiwa  kuwa Kajala anaweza kufungwa kwa kuwa hukumu inapitiwa upya.
Wakili wa Kajala, Peter Kibatala alisema anapambana kunyoosha sheria kuhakikisha mteja wake anakuwa huru.

Stori: Global Publishers
Wema Sepetu Kumlipia Kajala 13 Milioni Wema Sepetu Kumlipia Kajala 13 Milioni Reviewed by Admin on Wednesday, November 20, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.