Unordered List

Definition List

HUZUNI: NELSON MANDELA AMEKUWA BUBU!!!

Nelson Mandela
Mandela mwenye miaka 95 amekuwa akikumwana matatizo ya kiafya kwa muda mrefu na sasa imedhihirika kuwa rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini amelemewa na ugonjwa na uzee.

Kulingana na ripoti kutoka familia yake ya karibu, mkewe wa zamani wa Nelson Mandela Winnie Midikizela Mandela, ameiambia dunia kuwa Mandela hawezi kuzungumza na hutumia ishara ya uso ili kuwasiliana.

Nelson alikuwa akikabiliana na magonjwa ya mapafu hospitali Pretoria kwa muda wa zaidi ya miezi mitatu na alilazimishwa kurudi nyumbani mwezi wa Septemba.

Serikali ya Afrika Kusini inadai kuwa hali ya kiafya ya mkombozi huyu wa nchi ya Afrika Kusini kutoka minyonyoro ya ukoloni haijakuwa kitamu na kila wakati inazoroteka.
HUZUNI: NELSON MANDELA AMEKUWA BUBU!!! HUZUNI: NELSON MANDELA AMEKUWA BUBU!!! Reviewed by Admin on Monday, November 18, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.