Unordered List

Definition List

Wema Sepetu: Nimepotuza Mtu Muhimu Katika Maisha Yangu

wema sepetu
MWIGIZAJI wa kike wa filamu mwenye jina kubwa Bongo Wema Sepetu ‘Madam’ hivi karibuni alimpoteza baba yake mzazi aliyefariki katika Hospitali ya TMJ. Kufuatia msiba huo Wema alifunguka kwa kudai kuwa baba yake alikuwa ni kiungo muhimu sana katika harakati zake za urembo na sanaa kwa ujumla kwani baba yake alimuunga mkono katika kufanikisha ndoto zake.

“Nimepoteza mtu muhimu sana katika maisha yangu baba alikuwa akinisupport katika sana kwani hata awali nilipotaka kuingia katika mambo ya ulimbwende baba yangu aliniunga mkono, kulingana na nafasi yake kwa mzazi mwingine isingekuwa rahisi kunikubalia kuingia katika mashindano ya umiss,”anasema Wema.

Wema anasema hadi dakika za mwisho kabla ya baba yake kufariki alikuwa akimwita Miss World, hata alipoingia katika sanaa ya uigizaji wa filamu bado mzazi wake huyo alimuunga mkono jambo ambalo kwake lilikuwa ni faraja na kujivua kuwa na mzazi anayetambua umuhimu wa kipaji cha mwanaye.
Wema Sepetu: Nimepotuza Mtu Muhimu Katika Maisha Yangu Wema Sepetu: Nimepotuza Mtu Muhimu Katika Maisha Yangu Reviewed by Admin on Wednesday, November 13, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.