BAADA ya hivi karibuni staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ kueleza
mazito kuhusu Ray, Johari na Chuchu Hans, msanii mwenzake, Nuru Nassoro
‘Nora’ naye amefunguka kuwa laana ya walichomfanyia miaka ya nyuma
itawatesa Ray na Johari mpaka kifo chao.
Nuru Nassoro ‘Nora’.
Akizungumza na mapaparazi wetu hivi karibuni, Nora alisema Ray na Johari
walimfanyia ‘mambo mabaya’ yaliyosababisha kupotea kabisa kwenye sanaa
ya filamu hadi alipoibuka upya hivi karibuni.
Johari.
“Kinachowasumbua Ray na Johari ni laana yangu na kweli nimeamini Mungu
analipa hapahapa duniani kwani walinifanyia mambo ya ajabu, wakanipoteza
kabisa kwenye fani, walinifanya nichanganyikiwe wakijua sitapona,
lakini sasa hawaelewani tena wakati walikuwa wanapendana kama pete na
kidole.
“Nakumbuka zamani nilikuwa nikishonea nywele nzuri lazima Ray naye
akamnunulia Johari kama hizo za kwangu, alimtengeneza Johari akawa
anaigiza kama mimi na kujifanya yeye ndiyo mimi mpaka waliponipoteza
kwenye fani.
Ray.
“Namshukuru Mungu nimejikongoja na hatimaye nimerudi tena kwenye sanaa,
mabaya waliyokuwa wakinifanyia yamewarudia wenyewe, jamani mwacheni
Mungu aitwe Mungu kwani nakesha nikiomba na ninaamini maadui zangu wote
wataumbuka mchana kweupe,” alisema Nora.
Gazeti hili liliposhindwa kumpata Ray kwa kumpigia simu lilimtumia ujumbe ambapo alijibu kwa kifupi.
“Dah, kiukweli kama Nora ndiye kasema hivyo basi mimi sina comment yoyote na madai hayo na kirahisi naomba uandike hivyohivyo,” alijibu Ray.
“Dah, kiukweli kama Nora ndiye kasema hivyo basi mimi sina comment yoyote na madai hayo na kirahisi naomba uandike hivyohivyo,” alijibu Ray.
Kwa upande wa Johari alipotumiwa ujumbe aliendelea ‘kunyuti’.
CREDIT-GPL
Niliwalaani Ray Na Johari , Nora Apayuka
Reviewed by Admin
on
Thursday, November 28, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano