NABII Elisha Muliri wa kanisa la Ebeneza
mjini Dodoma ameingia matatani baada ya kudaiwa kumbaka na kumtia mimba mwanafunzi na kukatiza masomo yake huku kutishia
kumuua.
Akisimulia
tukio hilo mbele ya waandishi wa habari mwanafunzi huyo Martha Daniel [17]
kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya City iliyopo manispaa ya Dodoma
alisema kabla ya kufanyiwa kitendo hicho alikuwa anaangushwa na mapepo.
Martha
alisema baada ya kuhangaika kwa muda mrefu bila mafanikio walipata taarifa za
ujio wa nabii huyo mjini humo na wapofika ili kupata msaada wa kuombewa mapepo
hayo yalilipuka na binti akaponywa hata leo na kuahidiwa mbele ya kanisa
kusaidiwa ada na Nabii huyo.
Binti huyo
alisema baada ya kuponywa akaendelea kwenda kusali kanisani hapo ambapo
kutokana na kila mtu anayefika na kufanyiwa maombi huacha mawasiliono kwenye
vikaratasi, na Juni 8 mwaka huu majira akapigiwa simu na Nabii huyo akipewa
maelekezo ya kufika nyuma ya ukumbi wa Paradise ambapo walikuwa wakifanyia
ibada.
Mama Mzazi Mary Mkombola akiongea na wanahabari |
Anatanabaisha
kuwa baada ya kuonana Nabii alimwambia aingie kwenye Gari akaingia akifikili
kuna heri akapewa soda aina ya Fanta orange alipokunywa akapoteza fahamu na
alipokuja kuzinduka alijikuta akiwa nyumba za kulala wageni makole na Nabii
akiwa amemlalia kama alivyozali huku akiangalia mkanda wa Ngono.
Unaweza pia kusoma:
Mchungaji ashika sehemu nyeti za muumini
Unaweza pia kusoma:
Mchungaji ashika sehemu nyeti za muumini
"Wakati
nataka kupiga kelele alinitishia kwamba ataniua kama nitathubutu kumwambia mtu
yoyote jambo hilo, akanipiga kofi na kuniambia yeye hawezi kunilipia ada bure
kwa sababu mimi siyo ndugu yake lazima lazima alale na mimi mara 5 kwa hiyo
bado mara 4 na kunisisitiza asisikie popote kuwa alinifanyia hivyo", alisema
Mwanafunzi huyo.
Kwa upande
wake Mama mzazi wa mwanafunzi huyo Mary Mkombora alisema alimpeleka kuombewa
kutokana na kusubuliwa na mapepo tangu akiwa Darasa la sita na wakakubaliana na
Nabii huyo kumlipia ada kwa awamu hivyo akachukue 50,000 kila mwezi ili
kukamilisha 400,000 inayotakiwa shule.
Nilimgundua yupo
tofauti kuanzia mwezi wa saba nilipomuuliza alisema yeyue haelewi siku moja
nikamshuhudia akitapika asubuhi ndipo nilipochapa na kumfukuza nikapigiwa simu
na waliompokea kua mtoto kapewa mimba hiyo na Nabii kwanini nimemfukuza ndipo
nikachoka, alipopimwa alikuwa na mimba.
Mwanasheria Mfawidhi Mkazi wa kituo cha msaada wakisheria cha Tanzania Legal Aid Centre (TALAC), Godwin Ngongi akieleza kuhusu tukio hilo |
Alisema Nabii
huyo ambaye alikuwa Mume wa mwimbaji Marufu wa Nyimbo za Injili marehemu Anjera
Chibalonza kwa sasa hajulikani alipo japo mara kadha wasaidizi wa kanisa hilo
ambalo limebadilishwa jina kutoka Shakinah Pentecostal Church na kuitwa Ebeneza
wamekuwa akitaka Suruhu.
"Sasa hivi mimi na mtoto wangu tumekuwa
tukiishi mashakani baada ya Msaidizi wake Nabii Monica nimpe Martha akamtoe mimba kwa ataaramu anaowajua
wao, siku ambayo alichukua kadi yenye namba za simu na kufuta meseji zote
mwanangu alizokuwa akiandikiwa na Nabii,"
Nabii huyo
kwa sasa hajulikani alipo na hata alipotafutwa kwa simu yake ka mkono 0756
409118 ilikuwa amezimwa na msaidizi wake Nabii Monica Nyambura raia wa nchini Kenya
anakotoea Elisha Muliri alisema yeye hawezi kuongelea jambo hilo kwakua yeye ni
mgeni ameachiwa kanisa hilo baada ya mwenyeji wake kuwa safarini hivya
asubiliwe hatachelewa.
Tukio hilo
limefikishwa katika kituo cha sharia cha Tanzania Legal Centre [TALAC] na
mwanasheria mfawidhi mkazi Dodoma Godwin Ngongi tayali ameshamuandikia mkuu wa
kituo cha polisi kati barua ya kuwataka kumkamata mtuhumiwa huyo ili afikishwe
kwenye vyombo vya sharia na pia kuepusha mwanfunzi huyo na hatari nyingine.
Jeshi hilo
limekiri kuwa na taarifa ya tukio hilo na kwamba wanaendelea na uchunguzi
Chanzo: Pamoja Pure Blog
LAANA: Nabii Abaka Mwanafunzi Wa Shule Na Kumpa Mimba
Reviewed by Admin
on
Wednesday, November 13, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano