Unordered List

Definition List

Mimi Ndiye Niliyewaua Kanumba Na Sharo Milionea

Waumini wa kanisa la Powerful Gospel Ministy walishtuka baada ya jamaa mmoja alipojitikeza madhahabuni na kudai kuwa yeye ndie alihusika kutoa uhai wa wasanii watajika nchini Tanzania.

Mwanamume huyo aliyejitambulisha kama Mchungaji Mayanga alidai kuwa alisababisha vifo vya Hussein Ramadhan Mkiety 'Sharo' na Steven Kanumba 'The Great.

Ushuhuda huo ulitokea Jumapili iliyopita tarehe 13 mjini Dar es salaam sehemu za Mbagala-Charambe, Mzambarauni.

Jamaa huyo alipewa nafasi hio azungumzi hayo yote na Pasta wa kanisa hilo ajulikanae kama Meshak Punkanya.

"Nimesababisha vifo vya watu zaidi ya milioni 605 kupitia njia za kiza," alisema jamaa huyu. "Kabla sijaokoka nilikuwa nikifanya maovu mengi kwa kushirikisha nguvu za kiza ili kuangamiza watu. Nilikuwa mchawi mkubwa na uwezo wangu wakuangamiza watu ulikuwa sambamba na ule wa shetani mwenyewe lucifer, lakini sahizi nasikitika kwa yote niliyoyafanya." aliendelea kusema hayo.

Nchini Tanzania pekee, jamaa huyu alidai kuwa ni yeye ndiye aliyehusika kuangamiza wasanii wengi wakiwemo waimbaji wa taarab wa Kundi la Five Stars wapatao 14, Kanumba, Sharo Milionea na mwanamuziki James Dandu ‘Mtoto wa Dandu’. Pia jamaa huyo alikisia kuwa yeye ndiye alichochea kati ya vita dhidi ya Saddam Hussein na George Bush.
Steven Kanumba


"Nimekuwa nikitumia pepo kwa jina 'Magweju' ili kutimiza mauaji haya yote." alisemea huku akiliambia kanisa kuwa alihusika na janga la Westgate, mjini Nairobi Kenya.

'Mchungaji' huyu pia alikiri kuwa alijaribu kuwaonya wasanii kama vile Kanumba na Dumba akiwaambie waokoke kabla hajawaua. "Niliwatokea mara kadhaa nikiwashawishi wamrudie muumba wao lakini hawakuusikiza wito wangu." alidai kusema.


Sahizi jamaa huyu Mchungaji Mayanga ametabiri kuwa kuna siku moja lazima atakuja kukamatwa na kutiwa kizimbani kwa kuwa anajua siri nyingi za watu watajika nchini Tanzania. "Mimi najua siri nyingi za watu wanaotajika katika serikali na biashara na wengine wao mafanikio yao yote yametokana na nguvu zangu za kiza...nina siri nzito ambazo nyinyi hamuwezi huzistahimili." aliendelea kusema.
Sharo Milionea






Kwa sasa jamaa huyo ameachana na mambo haya yote ya kumtumikia shetani na ameamua kumrudia mungu wake kwa hivyo wasanii wasikuwe na shaka lolote kumhusu. 

Sharo Milionea alipatikana na ajali isiyoeleweka huku kanumba alifariki katika njia ambayo mpaka wa leo haijabainika vizuri
Mimi Ndiye Niliyewaua Kanumba Na Sharo Milionea Mimi Ndiye Niliyewaua Kanumba Na Sharo Milionea Reviewed by Admin on Friday, October 18, 2013 Rating: 5

2 comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.