Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ya watani wa jadi Simba na Yanga
iliyochezwa Jumapili (Oktoba 20 ) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam na kumalizika kwa sare ya mabao 3-3 imeingiza sh. 500,727,000.
Mashabiki
57,422 ndio waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo nambara 63 kwa
viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000
na sh. 30,000.
Kulibakia tiketi 131 tu ambazo hazikuwe kuuuzwa zikiwa 90 za VIP A, 40 za VIP B na
moja ya VIP C. Tiketi zilizochapwa kwa ajili ya mechi hiyo ni 57,558
ambayo ndiyo idadi ya viti vilivyopo kwenye uwanja huo.
Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,025,564.32 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,382,084.75.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 62,555,371.69,
tiketi sh. 7,309,104, gharama za mechi sh. 37,533,223.01, Kamati ya Ligi
sh. 37,533,223.01, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
18,766,611.51 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 14,596,253.39.
Unaweza pia Kusoma:
Fastjet Yaingia Katika Kumbukumbu
Unaweza pia Kusoma:
Fastjet Yaingia Katika Kumbukumbu
Boniface Wambura Mgoyo, Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) alitoa takwimu hii.
Mechi Ya Simba Na Yanga Yafaidi Zaidi Ya Sh 500,000,000
Reviewed by Admin
on
Tuesday, October 22, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano