Huku uchunguzi ukiwa bado unaendelea na maofisaa wa polisi, tetesi zimeanza kuibuka kwa nini mwanahabari wa ITV na Radio One alikumbwa na uvamizi na majambazi.
Kulingana na uvumi mwingine unaotufikia ni kuwa marehemu Atery Mushi aliandika barua kabla ya kufariki. Na barua hii ilieleza kwa nini alichukua hatua hio ya kujitoa uhai.
Inakisiwa kuwa Marehemu Mushi alikuwa na nyumba ambayo alimuachia Ufoo Saro na mamake waimiliki, lakini wakati Mushi alipokuwa nje ya nchi, Ufoo alibadilisha hati miliki ya nyumba hio na kuifanya yake.
Kulingana na ndugu wa marehemu Mushi ni kuwa kulikuwa na ugomvi mrefu kati ya Ufoo na Mushi kuhusu umiliki wa nyumba hio na kulikuwa na vikao zaidi ya vitatu bila mafanikio yeyote kutatua jambo hilo.
Kulingana na barua hio ambayo iko mikononi mwa polisi, mwendazake Mushi alieleza alichofanyiwa na hatua aliyoichukua kuhusiana na jambo hilo. Sasa haijulikani kama mwendazake Mushi alipanga uvamizi huo kabla kufariki au la.
Lakini uchunguzi wa swala liko mikoni mwa polisi na taarifa kamili kuhusu jambo hili litajulikana hivi karibuni.
Ufoo Saro baada ya upasuaji |

SIRI INAFICHUKA: Kwa Nini Ufoo Saro Alipatikana Na Majanga
Reviewed by Admin
on
Friday, October 18, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano