Unordered List

Definition List

Mama Alazimishwa Kula Kitoweo Cha Kuku Mbichi

Nairobi. Kulizuka kizaazaa katika kitongoji kimoja cha Ruai jijini Nairobi baada ya mama mmoja kulazimishwa kula kitoweo cha kuku mbichi.

Tukio hili lilitokea baada ya mama huyu kusemekana kuiba kuku wa jirani. Kulingana na watu wa mtaa huo, inasemekana kuwa mama huyo amezoea kupata riziki zake za kila siku kwa njia zisizo halali.

"Huyu mama amezoea kula asichopanda, leo lazima tumtie adabu." Jamaa mmoja aliongea huku akishikilia fimbo. Majirani waliogadhabishwa na matendo ya mama huyu walitaka kumtia adabu kwa kumlazimisha kula kitoweo cha kuku mbichi .

Mama huyu anayejulikana kama Veronica, alinaswa na majirani akiwa ameshikilia kuku. Baada ya kudhihirishwa kuwa huyo kuku amemuiba, alichukuliwa na kupelekwa hadharani. Alijaribu kuulizwa maswali lakini alikana. Jambo hili liliwaudhi majirani hao na wakaamua kumtia adabu. Bila ya kumpika au kumchemsha kuku huyo alilazimishwa kumla huku akipokea kichapo cha mbwa.



Mama huyu alijitetea asamehewe akieleza kuwa yeye ni mjane lakini ilikuwa kama kumpigia mbuzi gita. Hangeweza kujinasua kutokana na mambo yake aliyofanya.

Sehemu nyingi nchini humo watu wameanza kuomba misaada kwa wachawi ili kuwanasa wezi. Hivi maajuzi kuna kijana mmoja alipatikana akila nyasi na kulia kama ng'ombe baada ya kuaminika kuiba mali ya wa wenyewe. Mambo ya kiajabu kufanyika nchini humo mpaka siku hizi huonekana kama mambo ya kawaida.
Mama Alazimishwa Kula Kitoweo Cha Kuku Mbichi Mama Alazimishwa Kula Kitoweo Cha Kuku Mbichi Reviewed by Admin on Friday, October 11, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.