Unordered List

Definition List

CHRIS BROWN ATIWA MBARONI

Chris Brown ametiwa mbaroni baada ya kupiga shabiki wake.

Kulingana na habari zinazotoka kutoka TMZ, Chris Brown alianza kumpiga mangumi jamaa flani nje ya hotel ya W mjini Washington.

Inaaminika Brown hakuwa katika ulevi wakati wa tukio hilo.

Hivi tunavyoandika chapisho hili, msanii huyu ambaye alikuwa na mahusiano na Rihanna bado yuko korokoroni na aliyempiga ameachiliwa baada ya kupewa matibabu ya dharura.

Inajulikana kuwa Chris Brown yuko katika usimamizi(probation) kutoka mwaka wa 2009 baada ya kupigana na Rihanna.

Wakati huu akipatikana kama amekiuka utaratibu huo basi anaweza kufungwa kwa muda wa hadi miaka minne.

Kulingana na tukio hilo inasemekana mwanamke mmoja alitaka kupiga picha na Chris Brown ambayo alikubali.

Lakini kabla picha iweze kuchukuliwa, midume miwili ilitaka kujianika mbele ya picha hio ambayo ilimkasirisha Brown ndio mgongano ukaanza.

Msanii huyo alisikika akisema hivi' "Mimi si msenge bali niko katika ndondi" ambapo ndipo alimrushia muathiriwa huyo ngumi moja ya uso. Jamaa huyo hakujibu chochote.

Vita hivyo vilienda hadi chini na ilibidi polisi kuitwa ili kutatua mzozo huo.

Unaweza pia kusoma:
Rihanna akidengua kiuno nusu uchi(video)

Duru zinasema Jamaa huyo ameumizwa pua na anahitaji upasuaji. Amedai kuwa kesi hio haitaishia hapo na Chris lazima amlipe fidia.

Tegea hapa hapa kupata story inavyoendelea...
CHRIS BROWN ATIWA MBARONI CHRIS BROWN ATIWA MBARONI Reviewed by Admin on Monday, October 28, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.