miraa imehalalishwa rasmi nchini Kenya |
Mti huu ambao unakuzwa sehemu za Meru ulizua hisia nyingi baada ya nchi za ugaibuni huutaja kama dawa ya kulevya. Nchi kama uingereza na uholanzi ambazo zilikuwa nchi kuu za kusafirishwa mti huu waliupiga marufuku.
Jambo hili lilizua tetesi nyingi huku ikijulikana wazi kuwa mti huu hutoa mamilioni ya ushuru kupitia nchi za ngambo. Wabunge walifanya utafiti wao huku wakilieleza bunge kuwa mti huu una manufaa mengi kuliko madhara.
"Miraa ni mti ambao ni baraka na ulishukishwa na Mungu," mkaazi mmoja Meru alidai. "Miraa kwa kawaida yangu kila baada ya mavuno hutoa fungu la kumi kwa Mungu kumshukuru," aliendelea kusema.
Wanaharakati kadhaa waliitaka serikali kuuharamisha mti huu wakieleza kuwa vijana wengi wanapoteza wakati mwingi wakitafuna kama mbuzi na kuzunguza mambo yasiyoelewa.
Rais Uhuru Kenyatta alimpa jukumu mkuu wa NACADA Bw. Mututho kutatua jambo hilo. Siku ya Jumanne ilijulikana rasmi kuwa mti huu umehalalishwa na unaweza kutumiwa na kuuzwa kama vileo vya kawaida vinavyotumiwa nchini.
Miraa Yahalalishwa Rasmi Nchini Kenya
Reviewed by Admin
on
Thursday, October 10, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano