Unordered List

Definition List

Mwogeleaji Ajitetea Kwa Mangumi Baada Ya Kuvamiwa Na Papa

Jeff Horton alidhania atakufa wakati wa shambulio hilo
Mwogeleaji mmoja wa Hawaii ameponea chupuchupu baada ya kuvamiwa na papa.

Jeff Horton, 25, alikuwa akifanya mchezo wa 'surfing' kabla papa huyo kuonekana kwa maji.

Jeff alikuwa ameiweka miguu yake ndani ya maji kabla kuona kitu cheusi kikimsogelea.

Mwanzo jamaa huyu alidhania ni vitu vyeusi ndani ya maji mpaka alipomuona papa huyo ameuma bodi aliyokuwa ameilalia.

Papa huyo alikuja kwa nguvu na kuiuma bodi yake ya kuogelea na ilimfanya kumrusha, bahati nzuri aliweza kumshikilia papa huyo bawa lake la juu.

Hapo hapo Jeff alipata ujasiri na kuanza kumpiga papa huyo mangumi huku akijisaidia na mkono mmoja.

Unaweza pia kusoma:
Tunahitaji Amri 10 Za Musa Za Kisasa Ulimwenguni

Bidii yake ilimfanya kumpiga jicho lake moja ambalo lilimfanya papa huyo kuona kiza na kumuachilia.

"Nilifanya bidii mpaka nikafaulu kumpiga ngumi moja ya nguvu kwa jicho lake." Jeff aliongea.

Jeff aliweza kusaidiwa na mwenzake hadi ufuoni huku papa huyo akiwafuata polepole nyuma yao.


Mwogeleaji Ajitetea Kwa Mangumi Baada Ya Kuvamiwa Na Papa Mwogeleaji Ajitetea Kwa Mangumi Baada Ya Kuvamiwa Na Papa Reviewed by Admin on Thursday, October 24, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.