Unordered List

Definition List

Magari 10 Ambayo Yana Sura Mbaya 2013

Utafiti uliofanywa na Telegraph, walikusanya magari kumi ambayo yana sura mbaya ulimwengu mzima. Hii hapa ndio orodha ya magari haya kuanzia nambari ya kumi.

#10. Subaru Tribeca. Gari hili liliundwa mwaka wa 2005, likatengenezwa lionekane vyema mwaka wa 2008. Lina viti 5 hadi 7

#9. BMW X6. Huu ni mfano mzuri kwa nini usichanganye aina ya SUV na Coupe

#8. Rodius. Kama hili gari ukiliangalia na upande wa nyuma linatisha. Je ukiangalia na mbele si ni maajabu.

#7. Ford Scorpio. Hili gari limefananishwa kama chura aliefungua mdomo. Ni wazi kampuni ya Ford ilikuwa haijapanga kutengeneza gari aina kama hii.

#6. Paceman. Gari hili lilitengenezwa ili liwe gari mbadala ya Range Rover Evoque. Ina milango 5. Lakini mfanano wake na Evoque ni mbali sana.

#5. Subaru Impreza WRX. Hili gari liliundwa mwaka wa 2000. Lilitengenezwa na mtambo wa kawaida wa kampuni hii. Lakini kitu ambacho hawakuangalia ni mwili wake. Imetengenezwa na mwili wa 'sporty' lakini hivyo hivyo haijaridhisha.

#4.Fiat Multipia. Hili gari ni tofauti kwa sababu linabeba watu wasita katika mistari miwili. Hii imefanya kuwa pana kupitia kiasi, halafu rangi yake si ya mafuta.





#3. Yaris Verso. Hili gari ni zuri na lina wafuasi wake. Gari hili limetengenezwa kati ya 'supermini' na 'van', muundo wake ni mzuri lakini sura yake mbovu.

#2. Pontiac Aztek. Mwaka wa 2008, telegraph walitaka kujua gari lenye sura mbaya duniani na hili gari lililotengenezwa mwaka wa 2001-2005 lilichukua nambari ya kwanza.

#1. Jeep Cherokee. Hili gari limezua mijadala tofauti tofauti kwani halifanani na gari la kwanza la laini ya Cherokee.




Magari 10 Ambayo Yana Sura Mbaya 2013 Magari 10 Ambayo Yana Sura Mbaya 2013 Reviewed by Admin on Saturday, October 19, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.