Unordered List

Definition List

Shehena Inayomilikiwa Na Mwanasiasa Mashuhuri Yapekuliwa. Ndani Imepatika Na Vikaragosi Vinavyoaminika Kuwa Vya Uchawi

Mombasa. Wakaazi wa kisiwa cha Mombasa waliamkia kwa hofu na woga baada ya kupatikana shehena bandarini yenye vyombo vya kutisha.

Maafisaa katika bandari hio waliigundua shehena hiyo baada ya kufanya uchunguzi wa kawaida katika bandari hiyo.

Shehena hiyo inaaminika kutoka nchi ya Uchina na imekusudiwa kuingia jiji hilo.

Kati ya vitu vilivyopatikana ni fuvu za binadamu, miili ya wafu na masanamu ya kutisha ambayo imeaminika ingetumiwa kufanyiwa uchawi. "Mimi siamini mtu yeyote. Siwezi kujua kama mtu anaabudu Mungu au shetani." afisaa mmoja aliambia vyombo vya habari huku akiwa ameingiwa na kibaridi.

Afisaa mwingine aliyehojiwa na wanahabari alieleza kuwa baada ya kufanya uchunguzi ilibainika kuwa shehena hiyo inamilikiwa na mwanasiasa anayesifika sana nchini humo. "Tunaendelea na uchunguzi wetu kubainisha kwa nini shehena hii imeletwa humu nchini na ina matumizi gani." aliendelea kusema.

Wadadisi wanasema kuwa pengine huo ni ujanja umetumika ili kuzubaisha watu huku jambo lingine kuu likipangwa kufanywa. Uchunguzi unaendelea kubainisha chanzo cha haya yote.
Shehena Inayomilikiwa Na Mwanasiasa Mashuhuri Yapekuliwa. Ndani Imepatika Na Vikaragosi Vinavyoaminika Kuwa Vya Uchawi Shehena Inayomilikiwa Na Mwanasiasa Mashuhuri Yapekuliwa. Ndani Imepatika Na Vikaragosi Vinavyoaminika Kuwa Vya Uchawi Reviewed by Admin on Thursday, October 10, 2013 Rating: 5

1 comment:

  1. Wanasiasa huaga na tamaa nyingi. nadhani alikuwa anaongeza nguvu zake za kichawi

    ReplyDelete

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.