Unordered List

Definition List

Ne-Yo Na Celine Dione Wametoa Kollabo. Kuwa Wa Kwanza Kuisikiliza!

Neyo na Celine Dione Wametoa Kolabo 'Incredible'
Msanii mkongwe wa nyimbo za blues kwa mara ya kwanza ametoa nyimbo na msanii Celine Dione. Kollabo ya nyimbo hii inaitwa 'Incredible' na ni nyimbo ambayo iko katika albamu mpya ya 'Loved Me Back to Life' inayotarajiwa kutoka mwezi ujao siku ya 5 Novemba.

Ijapokuwa wawili hao kutoa kolabo inaonekana kama majanga(sauti zao haziingiliani) lakini ukiisikiliza vizuri utapata kujua kuwa ni nymbo bab kubwa. Hebu pata kuisikiliza hapa chini:

Celine Dion - Incredible ft. Ne-Yo


Celine Dione ameweza kuisifia nyimbo hii kama inayokugusa na kukueleza jinsi ulivyo wakati huo. Kiufupi inaeleza jinsi ulivyo.

"Nimeshukuru kuhusishwa na muimbaji Celine Dione, lakini haikuwa jambo rahisi kwangu." aliongea Ne-Yo wakati wa mahijiano. Msanii Ne-Yo amewahi kutoa Kolabo na wasanii kama Rihanna, Beyonce na Mariah Carey.

"Hii nyimbo sikuitarajia kabisa, ilikuwa ya kuchanganya akili, Celine angeweza kuitoa hii nyimbo akiwa peke yake kwani sauti yake naona haingehitaji kuongeza yangu." aliongezea Ne-Yo

Celine Dione ni msanii anayejulikana sana kutoa nyimbo ya 'Titanic' maarufu kama 'My Heart Will Go On'
Ne-Yo Na Celine Dione Wametoa Kollabo. Kuwa Wa Kwanza Kuisikiliza! Ne-Yo Na Celine Dione Wametoa Kollabo. Kuwa Wa Kwanza Kuisikiliza! Reviewed by Admin on Sunday, October 27, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.