Flora Mtegoa, mamake mwendazake Steven Kanumba anahuzunishwa sana na mchungaji George Kairuki. Mchungaji huyu kwa muda mrefu ametumia jina la marehemu Kanumba ili kujinufaisha.
Familia ya Kanumba wanadai jamaa huyu anaendelea kueneza uvumi kuwa star huyu wa filamu za bongo bado yuko hai. Mamake marehehemu aliongezea kusema jamaa huyu kutoka zamani wakati Kanumba alipofariki alikuwa akieneza uvumi na mambo ambayo hata familia yao walikuwa hawayajui.
Mama Kanumba anadai kuwa hivi karibuni Kairuki alijitokeza kwa kudai kuwa Kanumba hajafa na amemtumia fedha katika simu yake, na kusema kuwa karibu atamrudisha duniani na kuendelea na maisha yake jambo ambalo mama wa marehemu anapingana nalo kwa kusema kuwa yeye kwa imani yake anaamini kuwa mwanaye amefariki na hakuna miujiza mingine.
Unaweza pia kusoma jinsi jamaa alivyodai kuwa amewaua Kanumba na Sharomilionea
“Huyu mtu anayeitwa Nabii George Kairuki sijui anatafuta nini katika familia yangu, Kanumba alikuwa ni kipenzi cha watu na sisi sote tumeshuhudia hilo kama kweli yeye ana uwezo wa kumfufua amfufue watu wote watafurahi kipenzi chao kurudi kama anavyosema yeye, mimi simjui hata sura zaidi ya kumuona katika picha,”anasema mama Kanumba
Mama Kanumba anasema kuwa iwapo Kairuki ataendelea na tabia hiyo itabidi afanye utaratibu wa kumfungulia mashitaka na hata ikibidi kumfungulia mashitaka na kumfunga endapo ataendelea na tabia ya kutumia sana jina la Kanumba katika kujitafutia fedha na kutangaza maneno ya ajabu ajabu.

Steven Kanumba Yuko Hai!!!...Flora Mtegoa Anapinga Madai Hayo
Reviewed by Admin
on
Friday, October 25, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano