Maisha Yake Ya Awali
Wema Sepetu alizaliwa katika familia ya kidiplomasia na alikuwa wa mwisho kati ya dada wanne. Babake ni Ambassador Abraham Sepetu.
Mwanadada huyu mwenye sauti ya kuvutia na kupendeza alianza kufanya show tangu utotoni . Alikuwa akiperform drama katika shule aliyosoma iliyoko Dar es salaam.
Alizaliwa mwaka wa 1988 katika Dr. Andrew's Hospital huko Dar ea salaam.
Elimu
Wema alimaliza masomo yake ya msingi na secondari kuko Dar. katika shule ya Academic International. Aliongeza masomo yake ya juu katika chuo kikuu cha Limkokwing University, nchini Malaysia. Alisomea biashara.
Kazi
Wema aliingia katika nyanja ya filamu kwa vishindo alipotoa filamu ya 'Point Of No Return' mwaka wa 2007. Aliingiza kama bibi ya mume tajiri ambaye alikuwa akiwakandamiza wapenzi wake na kuwaua. Katika filamu hio Wema alifanya juu chini mpaka akaujeuza mwenendo wa bwana huyo. Filamu hii ilikuwa bomba na watu wengi walipendezwa nayo.
Wema alianza kutoa filamu kama vile Red Valentine, White MAria, Tafrani, Sakata, Crazy Tenant, Diary, Lerato, Dj Benny na Basilila. Filamu hizi zilimfanya apae juu na kusifika mno.
Urembo
Mwaka wa 2006, alivalishwa taji la kuwa Miss Tanzania. Tamasha hiyo ilifanywa katika Diamond Jubilee Hall mjini Dar es Salaam. Zaidi ya wanawake 20 kutoka miji yote ya Tanzania walishiriki. Aliibuka mshindi na kutuzwa gari aina ya Toyota Rav 4 na tiketi ya kushiriki katika Miss World.
Wema alisafiri hadi mjini Warsaw, Poland kushiriki katika Miss World 2006, lakini hakufanikiwa kufikisha wale 17 bora.

Biografia Ya Wema Sepetu
Reviewed by Admin
on
Sunday, October 13, 2013
Rating:
(k) nimependa filamu zake
ReplyDelete