Mombasa, Kenya. Shehe anayejulikana kwa misimamo mikali anayejulikana kwa jina Ramadhan Juma amenaswa na polisi mjini Mombasa baada ya kugunduliwa kuwa ni mchochezi kwa waumini wa dini ya kiislamu.
Shehe huyu alitiwa mbaroni siku ya alhamisi katika msikiti maarufu wa Masjid Musa, mtaa wa majengo jijini Mombasa.
Kulingana na mkuu wa polisi wilayani hio Aggrey Adoli, wamechukua hatua hio ili kupunguza uchochezi na kutaka waislamu wawe macho na wasikubali kamwe kuhusishwa na mambo ambayo yanaathiri usalama wa nchi. Inasemekana viongozi wanatumia misikiti kueneza chuki.
Msikiti wa Masjid Musa umemulikwa na serikali kwa muda mrefu huku tetesi zikienezwa kuwa msikiti huo ulikuwa ukiwasajili wapiganaji wa mgambo wa Al Shaabab, madai ambayo yalilaaniwa vikali na wakuu wa msikiti huo.
Kuhakikisha kuwa jambo hilo halitawahi kutokea tena, wasimamazi wa msikiti Masjid Musa wamewaonya viongozi wasitumie lugha chochezi ambazo zitaleta migogoro kati yao na serikali. Pia wametoa ilani kuwa yeyote anayetaka kutoa hotuba lazima awasiliane na viongozi hao.
Hivi majuzi imamu mmoja wa msikiti huo, Imam Rogo aliweza kuuliwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana na serikali haijachukua hatua yeyote kuangalia chanzo chake. Kisababisho hicho kilizua maandamano ambapo kanisa moja liliweza kuchomwa.
Siku ya Ijumaa (25 Oktoba) Aggrey Adoli alisema wameimarisha usalama katika msikiti huo huku wakihofia kunakuwa na machafuzi.

Waandamaji katika msikiti wa Musa baada imam Rogo kuuliwa |

Shehe Atiwa Mbaroni Baada Ya Hotuba Ya Uchochezi
Reviewed by Admin
on
Friday, October 25, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano