Wakili Gloria Alfred katika mahojiano na vyombo vya habari |
"Jana Kanye West aliweka wazi kuwa ana haki ya kuwashambulia wapigaji picha ambao watamkasirisha kwa kumuuliza maswali asiyoyapenda" aliendelea kusema wakili huyu maarufu katika ulingo wa usanii marekani.
"Anaona kuwa kushambulia paparazi ni haki yake. Kanye aliwaonya mapaparazi katika runinga kuwa mtu yoyote akivuka mipaka yale hayuko salama." aliendelea kusema wakili huyu katika mahojiano.
Wakili huyu anamuwakilisha mpiga picha Daniel Ramos ambaye alishambuliwa katika uwanja wa ndege wa Los Angeles mwezi wa julai.
Jumatano usiku West katika mahojiano ya runinga alijisifu kuwa yeye ni genius na hana haki mtu yeyote kusema hivyo, na kama yeye hakujitambulisha kuwa genius basi angekuwa akijindanganya yeye na mafans wake. Pia Kanye alisema kuwa yeye yuko tayari kuwalinda wapenzi wake pamoja na mtoto wake.
Wakili huyu kumjibu alisema kuwa Kanye ajitayarishe kwa sababu kibati cha kunyamazisha ukorofi kiko tayari naatakumbana na mkono wa sheria na atachukuliwa hatua ya ukiukaji wa haki za binadamu pamoja na ufunjaji wa sheria.
Kibati Cha Kunyamazisha Ukorofi Kiko Tayari, Wakili Amounya Kanye West
Reviewed by Admin
on
Saturday, October 12, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano