Picha ya Diamond na Wema Uchina |
Wiki mbili zilizopita kulikuwa na tetesi na udaku mwingi kuwa wawili hao wamekisiwa kuwa pamoja kwa mara ya pili.
Ijapokuwa kulikuwa na uvumi mwingi ambao ulichangiwa na wawili hao kuhusu uhusiano wao, hadi wa sasa hatuwezi kusema kama wamerudiana ama wameachana.
Kwa mara nyingine Diamond amefunguka kuendeleza uvumi huo. Akihojiwa na Risasi mjini Dar, msanii huyu alieleza mengi kati yake na Wema Sepetu.
Msanii huyu anaejulikana kupendwa na wanawake alieleza kuwa alipotoka nchi ya Malaysia kufanya shoo, alienda hadi Uchina ambapo alipokewa na mwanadada Wema. "Tukio hili lilinishangaza kwani sikuwa na uhusiano mwema kati yangu na mwanadada Wema tangu tulipoachana zaidi ya mwaka sasa" Diamond alikiri.
Baada ya mapokezi, Wema alimpeleka star huyo Diamond hadi hoteli moja ya 'five stars' huko Hong Kong. "Nilishindwa kujizuia upendo wake alionipa wakati wote nilipokuwa naye huko Hong Kong kwani aliufufua uhusiano wangu naye ambao ulikuwa umepotea kabisa.
Inajulikana kuwa Diamond aliachana na mwanadada huyu Wema Sepetu na kuchumbiana na Penniel Mungilwa aka VJ Penny ambaye mamake Diamond amebariki pendo lao. Lakini inavyoonekana ni kuwa Diamond moyo wake bado upo na Wema.
"Mimi ningependa kuwa na mtoto wa Wema." Diamond alifunguka zaidi wakati wa mahojiano hayo.
Uvumi ulizuka wiki mbili zilizopita baada ya Wema kupiga picha kadhaa akiwa na Diamond, nyingine zikionyesha wawili hao wakishikana kwa mahaba.
Unaweza pia kusoma:
Mamake Kanumba Atishia Wale Wanaodai Steven Yuko Hai
Diamond alipoulizwa kama ziara yake ya kuwa Uchina ilikuwa ya kutoa filamu ya 'Temptation' iliyoongelewa sana, Diamond alikuwa na haya ya kusema "Kama ulidhani ziara yangu nchini Uchina ilikuwa ya kutoa filamu, basi utaingojea sana, hakuna filamu yoyote."
Tetesi nyingine ambazo ziliibuka wiki iliyopita ni kuwa Wema alikuwa ameenda Uchina kujeuza ngozi yake. Hadi sasa Wema hajajitoa rasmi kuthibitisha uvumi huu.
Hadi mudaa huu hatima ya Penny VJ haijajulikana...hakuna mtu anayejua kama wameachana na Diamond ama yapi yanayojiri. Wadaku wa blogu hii watahakikisha wamekuletea yote yanayojiri katika mduara huu wa mapenzi kati ya Wema, Diamond, na Penny.
Diamond Afunguka: Wema Ni Nani Kwangu
Reviewed by Admin
on
Saturday, October 26, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano