Unordered List

Definition List

Recho Atamani Kuliwa Uroda Na Wakenya

Juma lililopita, wanamuziki wa Kigoma Allstars akiwemo Diamond Platnumz na wengine walikuwa mjini Mombasa, Kenya kwenye show ya sehemu ya ziara yao katika nchini za Afrika Mashariki. Pamoja na kupiga show kali,  kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini Kenya, Recho aliwatia aibu kubwa wasanii wenzake wakati wakiongea na waandishi wa habari baada ya show.

"Mwanamuziki wa Tanzania aliwashangaza waandishi wa habari pale alipoongea mbele ya camera kuwa alihitaji kuridhishwa kimapenzi,"mtandao wa Standard Digital News, SDE umeandika.

"Recho, aliyekuwa akiongea na waandishi wa habari baada ya show mjini Mombasa, alisema alihitaji mwanaume wa kulala naye usiku huo. Akifedheheshwa kwamba hitaji lake halikufaniwa, mwimbaji huyo maarufu kwa wimbo wake Upepo, aliwaponda waandishi na watu wengine waliokuwepo pale kuwa hawakuweza kum’handle’ mwanamke,"uliandika.

Mtandao huo uliongeza: Recho hakuwa msanii pekee aliyefedheheshwa usiku huo kwani mwenzake Maunda alionekana backstage akilia baada ya kuzomewa atoke jukwaani na umati.

Chanzo: Standard Media
Recho Atamani Kuliwa Uroda Na Wakenya Recho Atamani Kuliwa Uroda Na Wakenya Reviewed by Admin on Tuesday, December 17, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.