Msanii huyo filamu na muziki kutoka Tanzania Baby Joseph Madaha, ameiambia Global Publishers kuwa mwanzoni yeye na Kariuki hawakuwa na uhusiano wa kimapenzi zaidi ya kazi, ila kutokana na watu kuanza kuongea kitu ambacho hakipo ndio kilichopelekea kuamua kufanya kweli,
“Kusema kweli huyu kaka kanikoleza jamani japo watu watachonga mengi lakini abadani sitosikiliza maneno yao, kwa kuwa awali sikuwa na uhusiano naye ila porojo za watu zilipelekea kuchukua maamuzi hayo, natamani nihamie Kenya ili tuwe karibu wakati wote,”alisema Baby Madaha.
Novemba 5 mwaka huu Baby Madaha alizungumza na Bongo5 na kukana tetesi zilizokuwepo wakati huo za uhusiano kati yake na Kariuki.
“Joe amesikia na hajapenda hili swala kwasababu sisi tupo kikazi zaidi na siyo mambo mengine kama wasemavyo wao”, alisema Madaha katika mahojiano hayo.
Madaha pia ameongeza kuwa ameamua kuwa na Kariuki kutokana na upendo anaomuonesha na si uwezo wa kipesa kama wengi wanavyodhani.
Baby Madaha Afungua Moyo Wake Zaidi: Mapenzi Yake Na Manager Wake
Reviewed by Admin
on
Tuesday, December 17, 2013
Rating:
No comments:
Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!
Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano