Unordered List

Definition List

Kanye West: Kim Kardashian Ni Genius, Atamshinda Beyonce Katika Mziki

Nani hamjui Kanye West, msanii ambaye anajiona kuwa yeye ni yeye. Kanye kwa sasa anaendelea kujifananisha na kila shujaa na hivi karibuni ametamka kuwa yeye ndiye atakayekuwa Nelson Mandela.

Kanye pia ashawahi kutamka kuwa yeye anataka aangaliwe kama mungu. Pia ameshawahi kujifananisha na Yesu na sasa anafanya tour anayoiita Yeezus. Kiufupi msanii Kanye anatafuta kila mbinu kuhakikisha umaarufu wake umerudi hivi ni baada ya utafiti kuonyesha kuwa msanii huyu amepungua umaarufu wake.

Hivi sasa staa huyu ameamua kuwaingilia Beyonce na Jay Z, huku akidai kuwa yeye na Kim Kardashian watakuwa wakiongoza katika nyimbo za rap.

Akiongea na WGCI radio, Kanye  ameapa kuwa atawangoa Jay Z na Beyonce katika game ya Hip Hop na atahakikisha kuwa yeye na Kim watatajwa kuwa couples wa hiphop.

Kim kwa sasa ameanza kuchukua vilasi vya kujifunza nyimbo na ameshajitokeza katika video moja na Kanye ambayo alionyeshwa akiwa nusu uchi juu ya pikipiki.

Beyonce akae chonjo kwa spidi ya Kim ambayo ameanza kuja nayo
Kanye West: Kim Kardashian Ni Genius, Atamshinda Beyonce Katika Mziki Kanye West: Kim Kardashian Ni Genius, Atamshinda Beyonce Katika Mziki Reviewed by Admin on Saturday, December 14, 2013 Rating: 5

No comments:

Tunapenda kuyasoma maoni/reaction kutoka kwako!

Kama una maoni tofauti na chapisho la hapo juu, wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano

Powered by Blogger.